Latest News 16 Oct 2019

News Images

VIKAO VYA UHAKIKI NA UKAGUZI MIRADI Z.VICTORIA

Vikao Vya uhakiki na Ukaguzi Miradi ambavyo hufanyika kila mwezi kati ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya serikali inayotendelea katika Z.Victoria na timu maalumu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano -Sekta ya Uchukuzi pamoja na wataalamu kutoka Kampuni ya Huduma za Meli vimenza kwa uwakilishaji ripoti ya Mwezi wa tisa.

Mara hii kikao hiki kimehudhuriwa na Msajili wa bodi ya Wahandisi kutoka Bodi ya usajili Wahandisi Tanzania (ERB)Mhandisi Patric Balozi.

Kawaida vikao hivi hufanyika ndani na nje kwa maana ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi lakini pia uhakiki wa kile kwa maelezo kama kinaoana na uhalisia.

Kikao cha kwanza ni kati ya Mkandarasi wa Chelezo ambaye ni Kampuni kutoka Korea ya Kusini Stx Engine akishirikiana na Saekyung naye kutoka nchini Korea ya Kusini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli ndugu Eric Benedict Hamissi amemuhimiza Mkandarasi kuongeza nguvu kazi ,hata kama ratiba yake inaonyesha kuwa ndani ya muda lakini ajitahidi kuongeza Vifaa vya utendaji pamoja na kufanya kazi ikiwezekana usiku na mchana ili kujihakikishia kukamilika kwa mradi huo mapema kabla ya muda ulio kwenye ratiba.

Hiki ni kikao cha mkandarasi wa mradi mmoja kati ya minne inayoendelea kutekelezwa katika Z.Victoria.

Pamoja na Chelezo miradi mingine ni Ujenzi wa Meli mpya ambayo mkandarasi wake ni GAS ENTEC kutoka Korea kusini akishirikiana na KANG NAM nayo kutoka korea Kusini pamoja na SUMA JKT ya Tanzania.

KTMI wao ni wakandarasi wa ukarabati mkubwa wa meli za MV.Victoria na MV.Butiama ambao wanashirikiana na Songoro Marine.

Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano Kampuni ya Huduma za Meli.