Latest News 02 Oct 2025

MAANDALIZI YA UJENZI WA KIWANDA CHA KUJENGEA MELI KIGOMA YAFIKIA PAZURI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) Ndg. Eric Hamissi pamoja na timu yaje ya wataalamu leo hii tarehe 10.09.2025 amekutana na Mkarandarasi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kujengea meli Dearsan Shipyard ya nchini Uturuki kuzungumzia maendeleo ya maandalizi ya ujenzi wa Kiwanda hicho katika eneo la Katabe Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkoani Kigoma.
Akizungumza katika kikao hicho Ndg. Eric Hamissi amesema kuwa barabara ya Kilometa moja kuelekea katika eneo la ujenzi wa kiwanda ipo katika hatua za mwisho kumalizika huku miundombinu ya umeme na maji ikiwa imeshafika katika eneo hilo.
Aidha Mkandarasi ameanza maandalizi ya kusafisha eneo la ujenzi pamoja na kuanza kujenga Cofferdam ambao ni uzio unaozuia maji katika eneo la ziwa ili kuwa na bwawa la muda.