Latest News 02 Oct 2025

WANAFUNZI CHUO CHA TENGERU WASIFU UJENZI MV. MWANZA
Wanafunzi wapatao 120 wa Shahada ya Uzamili kutoka wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wamesifu ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanafunzi hao wamesema kuwa mradi huo ni maono katika maandalizi ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050 na wananchi hupata hamasa ya kuendelea kutoa kodi pindi wanapoona umuhimu wa miradi hiyo katika kuimarisha Uchumi wa nchi.
Ziara hiyo ya kutembelea mradi wa MV. Mwanza ni sehemu ya utekelezaji wa masomo kwa vitendo kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa nchini. Mradi wa MV. Mwanza umefikia asilimia 98 ya utekelezaji ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2025