Latest News 15 Jun 2022

Miradi ya Ukarabati ya MV Umoja na MT Sangara yaendelea kupokea vifaa.
Miradi ya Ukarabati inayohusisha meli inayobeba mizigo ya MV Umoja inayofanya shughuli zake Ziwa Victoria pamoja na meli inayobeba mafuta ya MT. Sangara inayofanya shughuli zake Ziwa Tanganyika imeendelea kupokea makontena yenye shehena za vifaa mbalimbali vinavyohusisha kubadili mifumo mbalimbali ya meli hizo kutoka mfumo wa zamani wa analogia na kuwa katika mfumo wa kidigiti.
Makontena hayo yaliyotoka bandari ya Dar es Salaam yamepokelewa katika siku tofauti katika wiki ya kuanzia tarehe 6 hadi 10 ya mwezi Juni, 2022 yakiwa na vifaa tofauti huku Kontena lililowasili Bandari ya Kigoma likiwa na vifaa vya mfumo wa umeme huku kontena lililowasili katika Bandari ya Mwanza Kusini likiwa limesheheni vifaa vya kisasa vya mfumo wa mawasiliano kwaajili ya kuwekwa katika chumba cha kuongozea meli.
Mradi wa ukarabati wa meli ya MV Umoja unatekelezwa na kampuni ya SM Solution kutoka Korea Kusini na kutarajiwa kukamilika baada ya miezi 15 hadi kukamilika kwake itagharimu shilingi bilioni 19.8 inatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba makontena 21 badala ya uwezo wa sasa wa kubeba makontena 19. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2023.
Mradi wa ukarabati wa Meli ya MT. Sangara unatekelezwa na Kampuni ya KTMI kutoka Korea Kusini na Kutarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 na hadi kukamilika kwake itagharimu shilingi bilioni 8 na kubebe lita 410,000 ambayo ni sawa na tani 350. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2022.