Latest News 02 Oct 2025

BODI TASHICO YATEMBELEA MV. MWANZA
Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) imefanya ziara ya kukagua maendeleo ya hatua za mwisho za ufungaji fanicha ndani ya meli ya MV.New Mwanza.
Katika ziara hiyo ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mej.Jen.Mstf.John J.Mbungo amefurahishwa na hatua iliyofikia sasa ya kukamilisha ufungaji wa fanicha ambazo awali ndizo zilikuwa zikisubiriwa ili meli hiyo ianze safari zake.
"Tumekuja kuhakiki shughuli zinazoendelea hapa katika meli hii, mtakumbuka kwamba meli hii imeshakamilika upande wote wa mitambo kwa maana ya injini na Jenereta lakini pia zile sehemu za kukaa abiria. Mara ya mwisho tulikuwa tukisibiri vitanda na kabati za kutunzia mizigo abiria pamoja na baadhi ya fenicha za vyumbani ambazo tayari zilishafika zipo katika eneo la kazi na sasa zinaendelea kufungwa. Ni matumaini kufikia Septemba watakuwa wamemaliza hatua hiyo na meli itaanza safari zake za majaribio ya awali kusafiri kwenda Bukoba kabla ya kuzinduliwa rasmi" - Mej.Jen.Mstf.Mbungo.
Ziara hii imefanyika leo Agosti 19 ambapo vikao vya Bodi hiyo vinaendelea Makao Makuu ya TASHICO Mwanza.