Latest News 10 Dec 2019

News Images

MIRADI YENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 152 YAWEKEWA MAWE YA MSINGI Z.VICTORIA

Miradi Minne yenye Tamani ya Zaidi ya shilingi Bilioni 152 Imewekewa Mawe ya Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Miradi hiyo ni ile inayosimamiwa na Kampuni ya Huduma za Meli na Kutekelezwa katika Bandari ya Mwanza kusini ambapo ni Miradi inayohusisha Usafiri kwa njia ya Maji.

Miradi iliyowekewa mawe ya Msingi ni Ujenzi wa Meli Mpya ,Ujenzi wa Chelezo na Ukarabati Mkubwa wa Meli za MV.Victoria na MV.Butiama

Wakandarasi wa Miradi hii ni Kampuniya GAS Entec ambayo ndiyo Mjenzi wa Meli Mpya akishirikiana na KANG NAM zote kutoka Korea ya Kusini,Pamoja na SUMA JKT ya Tanzania.

Mradi huu utagharimu Shilingi Bilioni 89 pesa za Kitanzania.

STX Engine akishirikiana na SAE KYUNGU wote kutoka Korea ya Kusini hawa ni wakandarasi wa Chelezo.

Gharama za Mradi ni shilingi Bilioni 36

Mkandarasi wa Ukarabati wa Meli za MV.Butiama na MV.BVictoria ni KTMI nayo kutoka Korea ya Kusini.

Miradi hii itagharimu shilingi Bilioni 22.7 kwa Ukarabati wa MV.Victoria na Shilingi Bilioni 4.9 ukarabati wa MV.Butiama.

Miradi mitatu ya Ujenzi wa Chelezo na Ukarabati wa MV.Victoria na MV.Butiama hii inatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa Mwezi Mach mwaka 2020 ambapo Meli Mpya itakabidhiwa Mwanzoni mwa Mwaka 2021.