Latest News 25 Nov 2019

News Images

MELI MPYA KUITWA MV.MWANZA HAPA KAZI TU

Meli mpya inayojengwa katika Ziwa Victoria ambayo inatokana na ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli imepata Jina rasmiambalo ni MV.MWANZA HAPA KAZI TU.

Jina hilo limetangazwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa Jijini Mwanza ambapo kwanza alitoa Ufafanuzi kwanini wameamua kuiita MV.Mwanza na Si jina ambalo wengi walipendekeza ambalo ni la Mheshimiwa Rais Magufuli

’Nilipofika hapa pia niliuliza Meli hii mnapendekeza tuiite jina gani ? Wote wakasema MV.Magufuli.. SasaMimi nimejaribu kuongea naye lakini amekataa na kusema litafutiwe Jina lingine’’

Amesema Jina hili Limetolewa na Serikali baada ya Kamati maalumu ambayo hutumiwa na Serikali kuchakata majina,ndiyo iliyopendekeza Meli hiyo mpya kuitwa MV.Mwanza Hapa kazi tu

MV.Mwanza ni meli mpya inayojengwa katika Ziwa Victoria kwa gharama ya shilingi Bilioni 89 kwa kutumia pesa za walipa kodi watanzania , na itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na mizigo tani 400.

Ni meli kubwa kupita zote kwa sasa katika ukanda wote wa maziwa Makuu.