Latest News 07 Jan 2020
KATIBU MKUU UCHUKUZI AHIMIZA MANDALIZI BANDARI Z.VICTORIA KABLA YA SAFARI ZA APRIL
Dkt.Leonard Chamuriho katibu mkuu Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi akiwa ziarani Bandari ya Mwanza kusini Kukagua maendeleo ya Upanuzi wa Bandari lakini pia uongezaji kina cha maji sehemu ambazo ni Maandalizi ya eneo la kupaki Meli zinazorejea katika utoaji Huduma Z.Victoria ametoa agizo la kukamilika kwa wakati maboresho ya Bandari zote ambazo zitahusika katika Huduma zitakazoanza kurejea Mapema mwezi wa nne
Aidha ziara hiyo ilihusisha pia Ukaguzi hatua za maendeleo ya Miradi ya Meli ambayo husimamiwa na Kampuni ya Huduma za meli na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji ambayo kwa mujibu wake anasema inampa taswira ya kukamilika kwa wakati mapema mwezi Marchi 2020
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Meli mpya, Ujenzi wa Chelezo,Ukarabati wa Meli ya MV.Victoria pamoja na ukarabati wa MV.Butiama
Miradi yote mitatu itakayokamilika mwezi wa tatu ipo zaidi ya asilimia 75.Jumla ya Fedha zote za kukamilisha miradi hii ni Shilingi Bilioni 153 pesa zote ni za serikali ya Tanzania.