Latest News 18 Oct 2019
JENERETA NNE MPYA ZITAKAZOFUA UMEME WA INJINI MPYA NNE KATIKA MV.VICTORIA ZAFUNGWA RASMI KWENYE MV.VICTORIA
Zoezi la kupandisha Jenereta nne Mpya ambazo zitakuwa zikisaidia kufua umeme katika Injini nne Mpya zitakazofungwa katika Meli ya MV.Victoria tayari limekamilika.
Jenereta hizo zilizowasili nchini kutoka nchini Korea ya Kusini ni muendelezo wa kuwasili vifaa vipya vinavyofungwa katika meli hiyo ambayo ukarabati wake ni Mkubwa na wakipekee tangu kuundwa kwa meli hiyo.
Njia iliyotumika kupandishwa Jenereta ni yakutumia Winchi kupitia juu sehemu ya mwisho kwa urefu wa meli.
Mkandarasi wa Meli hiyo ni Kampuni ya KTMI inayoshirikiana na Yukos Enterprises pamoja na Songoro Marine ya Tanzania.
Mkandarasi anatekeleza miradi miwili ambayo ni Ukarabati Mkubwa wa MV.Victoria ambao thamani yake ni Shilingi Bilioni 22 na Ukarabati wa MV.Butiama ambayo unatumia shilingi Bilioni 4.9