Dira na Dhamira

DIRA

Kuwa Kampuni inayoongoza kwa huduma za usafiri wa majini zenye ushindani, tegemeo na zenye kumjali mteja katika ukanda wa maziwa makuu.

DHIMA

Kutoa huduma ya usafiri yenye kuongoza, inayotegemewa, ya uhakika, endelevu na salama kibiashara katika kuhudumia vizuri wateja wake katika maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

MAADILI YA MSINGI

USALAMA

Usalama ni utamaduni wetu; umeunganishwa katika kila sehemu ya shughuli zetu.

UADILIFU

Watumishi wa TASHICO daima tutaangalia na kudumisha viwango vya juu vya maadili na kujiepusha na upendeleo katika utoaji wa huduma na kuzingatia utawala wa sheria.

USHIRIKIANO

Watumishi wa TASHICO tunahakikisha tunatoa matokeo chanya, kufanyakazi kwa ari na kushirikiana wakati wote ili malengo ya Kampuni yafikiwe.

THAMANI KWA MWENYE HISA

Watumishi wa TASHICO tunafanya kazi ili kutoa thamani bora kwa uwekezaji na kurudisha gawio serikalini.

RAFIKI KWA MAZINGIRA

TASHICO wakati wote hutetea ulinzi wa mazingira kwenye maeneo inapofanyia kazi.