Latest News 24 Jun 2019

News Images

ZIARA YA WAZIRI WA UCHUKUZI KUKAGUA MAENDELEO MIRADI YA MSCL Z.VICTORIA

Tarehe 21/06/2019 Mh.Waziri wa Ujenzi, mawasiliano na uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe alitembelea na kukagua utekelezaji miradi ya Serikali katika Ziwa Victoria inayosimamiwa na Kampuni ya huduma za meli nchini.

Jumla ya miradi minne imekaguliwa ambayo ni ujenzi wa meli mpya,ujenzi wa chelezo,ukarabati mkubwa wa MV.Victoria pamoja na ukarabati wa mv.butiama.

Mh.Waziri amempongeza afisa mtendaji mkuu kampuni ya huduma za meli nchini ndg.Eric Benedict Hamissi kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji miradi, lakini pia tangu kuteuliwa kwake kusimamia kampuni hii Picha ya kufufuka kwa kampuni ya huduma za meli imeanza kuonekana.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella yeye ameshukuru uwepo wa utekelezaji miradi hii hapa Mwanza kwani ni fursa tosha kwa ajira na kupata uzoefu wa shughuli kwa wakazi wa eneo hili.

Yapo maelekezo yaliyotolewa na Mh. Waziri kwa mkadarasi wa ujenzi wa Chelezo Maelekezo STX Engineering ambayo Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za meli amemuelekeza mkandarasi kuzingatia agizo la Mh.waziri ili kuondoa mkwamo wowote katika ukamilikaji mradi kwa wakati.

Miradi yote hii itakamilika mwaka 2020

Zaidi ya shilingi bilioni 58 pesa za kitanzania zimesha lipwa na serikali ikiwa ni fedha zake kutokana na matunda ya kodi ya watazania

Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano – Kampuni ya Huduma za meli nchini.