Latest News 02 Jul 2019
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI NCHINI.
Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Atashasta Nditiye ametembelea Makao makuu ya kampuni ya huduma za meli nchini yaliyopo Mkoani Mwanza.
Mh.Nditiye amepokea taarifa ya utekelezaji maendeleo ya Miradiya Serikali inayosimamiwa na kampuni hiyolakini pia kusikiliza changamoto wanazokutana nazo wakati huu wa utekelezaji miradi hiyo.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli ndugu Eric Benedict Hamissi amemuhakikishiaMh. Naibu waziri kwamba miradi yote ipo katika asilimia nzuri kiutekelezaji na itakamilika kwa muda muafaka kama makubaliano yalivyo.
Miradi inayotekelezwa ni pamoja na Ukarabati mkubwa wa meli ya Mv.Victoria,Ukarabati mkubwa wa Mv.Butiama ,Ujenzi wa Chelezo(sehemu itakayotengenezewa meli Mpya) pamoja na Ujenzi wa Meli Mpya .
Jumla ya fedha zinazotekeleza miradi hii ni shilingi billion 152 fedha zinazotokana na kodi ya watanzania kwa asilimia mia moja.
Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano – Kampuni ya Huduma za Meli Nchini