Latest News 20 Jul 2019

News Images

KONTENA ZA VIFAA VYA MIRADI YA MELI Z.VICTORIA ZAFIKA MWANZA

Kontena zilizokuwa zimekwama Dar – es - salaam kwa kusubiri msamaha wa kodi tayari zimefika Mwanza katika eneo la Mradi ili kuendeleza kasi utekelezaji miradi

Kuwasili kwa Kontena hizi siku ya leo kunatokana na agizo la Mh.Rais akiwa ziarani mkoani Mwanza baada ya kutembelea eneo la miradi na kutaka kuhakiki Maendeleo ya Miradi ya Meli Z.Victoria na kupata maelezo ya kuchelewa kwa Vifaa vya Miradi ,kitendo ambacho kinaweza kuathiri kasi ya utekelezaji Miradi hiyo

Mh.rais aliagiza wizara zenye dhamana kushughulikia suala hilo kwa haraka na kuhakikisha vifaa vinafika Mwanza kufikia tarehe 20/07/2019 (siku ya leo) ambapo agizo hilo lilitolewa tarehe 16/07/2019

Miradi inayotekelezwa Z.Victoria ni Ukarabati Mkubwa wa Meli za MV.Victoria wenye gharama ya shilingi Bilion 22, Ujenzi wa Chelezo wenye gharama ya sh.bilion 36 cha wakati Ule mradi wa meli mpya utagharimu kiasi cha shilingi billion 89 na Ukarabati mkubwa pia wa MV.Butiama wenye kiasi cha billion 4 jumla ya fedha zote ni billion 152 fedha za walipa kodi.

Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano – Kampuni ya Huduma za Meli Nchini