Habari Mpya 19 Nov 2026
UCHUNGUZI MV. MWANZA KUFANYIKA
Serikali imesema inakusudia kuunda timu maalumu ya wataalamu kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali ya meli ya MV New Mwanza kugonga mwamba wa mawe maarufu kama Bismarck Rock, katika Ziwa Victoria jijini Mwanza.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 4:00 asubuhi wakati meli hiyo ikiwa katika majaribio ya kiufundi, huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Hamduni akithibitisha kuwa chombo hicho kiko salama na hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa muda mfupi baada ya tukio hilo, Hamduni amesema meli hiyo ilikuwa imeegeshwa kwa muda mrefu na TASHICO ilikuwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya kurejesha safari zake za kawaida.
"Meli iko salama. Majaribio yaliyokuwa yakifanyika leo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kiutendaji unaosimamiwa na wataalamu wetu wa TASHICO na si mara ya kwanza kwa zoezi hili kufanyika," amesema Hamduni.
Hata hivyo, amebainisha kuwa ili kujiridhisha na usalama wa chombo hicho kabla ya kuanza
