Latest News 27 May 2019
AGIZO LA AFISA MTENDAJI MKUU KWA KANDARASI WA MELI MPYA Z.VICTORIA
Afisa mtendaji mkuu Kampuni ya Huduma za Meli nchini Ndugu Eric Benedict HamissiAmeagiza uingizwaji Conteiner za Vyuma vitakavyotumika kujengewa Meli mpya vipitie katika Bandari yetu ya Dar –es – salaam na pia Reli yetu ya kati hadi Mwanza na si njia nyinginezo
Amesema hakuna sababu yoyote ya kupindisha hilo kwani Bandari yetu inauwezo wa kuhimili mzigo huo kwa wakati na pia Reli yetu inauwezo wa kufikisha mzogo huo Mwanza kwa wakati
Jumla ya container mia tatu(300) zenye ukubwa wa futi40 zinataraji kuanza kuingia nchini kati ya mwezi August Mwishoni na September
Ameyazungumza hayo katika kikao cha Pamoja kati ya Mkandarasi kutokaKorea KusiniGas Entecambaye ndiyemjenzi wa Meli hiyo Mpya ambayo tayariinaakisi jina la mh. Rais Magufuli (Meli ya Magufuli) walipokuwa Mwanza kwa mara ya kwanza katika ukaguzi wa sehemu itakapojengewa Meli hiyo
Hii ilikuwa ni hatua ya tatu ambapo tayari ujenzi wa Meli hiyo ulishaanza nchini Korea ya Kusini kwa hatua ya kwanza ya Michoro ambayo ilikamilika na kupitishwa na Jumuiya ya Kimataifa inayosimamia viwango vya ujenzi wa Meli Duniani(Lloyd Registry-UK) na pia kuthibitishwa na Wataalamu wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania
Hatua ya pili ilikuwa ni ukataji vyuma vya meli na uagizaji vifaa muhimu kama Injini kutoka kwa watengenezaji mashuhuri wa vifaa hivyo Duniani. Awamu iliyoanza mwezi May 2019 na itakamilikakatikati ya mwezi Jun2019 ambapo vifaa vyote sasa vitakuwa tayari kusafirishwa
Baada ya kuwasili vifaa vyotevinavyo hitajika, ambavyo vinataraji kufika kati ya mwezi August na September 2019 utekelezaji wa uunganishaji vyuma utaanza na hapo utachukua miezi 12.
Meli hii inataraji kukabidhiwaSeptember 2019